Vijana wafanya kampeni ya amani Lamu
1 Agosti 2014Mtandao wa Vijana katika kaunti ya Lamu huko pwani ya Kenya, Lamu County Bunge Network, umeanzisha kampeni ya kushajiisha wananchi wa jimbo hilo kuhusu amani. Kampeni hiyo iliyopewa jina - "We are One - yaani Sote Ni Wamoja" - ilianza rasmi Julai 21 mwaka huu na tayari imefanyika katika miji ya Mpeketoni, Witu, Mokowe na Shela katika kisiwa cha Lamu. Vijana wa mtandao huo wamekuwa wakihubiri amani kupitia maonyesho ya mabarabarani na mikutano ya hadhara katika miji mbalimbali wakitumia tingatinga moja walilopewa na serikali ya kaunti ya Lamu, kwa kuwa baadhi ya maeneo hayafikiki kwa kutumia magari kutokana na hali mbaya ya barabara. Josephat Charo amezungumza na Mwenyekiti wa Mtandao huo wa vijana, Michael Kanja, ambaye kwanza anaelezea kuhusu kampeni hiyo. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Josephat Charo
Mhariri: Mohammed Khelef