Huku Ethiopia ikiwa na mojawapo ya chumi zinazokuwa kwa haraka zaidi duniani, nchi hii imekuwa sehemu ambayo teknolojia inathaminiwa sana. Lakini imekuwa vigumu kwa vijana kujiajiri kwa kuanzisha biashara zinazohusiana na teknolojia kutokana na vigezo vingi upande wa serikali na ukosefu wa mtaji.