1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifo vya watoto vyaongezeka Botswana

Jane Nyingi22 Juni 2007

Japo kuwa taifa la Botswana limefanikiwa kupunguza kiwango cha umaskini, ni vigumu kutimiza lengo la nne la maendeleo ya milenia la umoja wa mataifa ambalo ni kupunguza idadi ya vifo vya watoto kwa thuluthi mbili kufikia mwaka 2015.

https://p.dw.com/p/CHkS

Tarakimu zimeonyesha ongezeko la vifo vya watoto katika kipindi kati ya miaka ya 90 na ya 2000.Ripoti iliyotolewa na afisi ya serikali kuhusu takwimu za watu na makaazi nchini humo, vifo va watoto waliochini ya miaka mitano limekuwa jambo la kawaida. Mwaka wa 2001 watoto elfu moja waliozaliwa, 56 kati yao walifariki. Katika muda sawa na huo hali iliendelea kuwa mbaya zaidi kwani vifo hivyo vilitoka watoto 63 kati ya elfu moja wanaozaliwa hadi 74.

Cha kustaajabisha zaidi ni kuwa tarakimu zilizotolewa na hazina ya watoto ya umoja wa mataifa kuhusu idadi ya watoto wanaofariki hata ni za kushtusha zaidi kwani ni tofauti kabisa na zile za serikali ya Botswana. Hazina hiyo inasema idadi kubwa ya watoto wanaofariki hasa ni kutokana na ugonjwa wa ukimwi.

Fatma hamisi muunguzi daraja la kwanza anayehudumu katika hospitali mmoja nchini Botswana anasema kutokana na maambukizi ya juu ya ugonjwa wa ukimwi nchini humo serikali ilianzisha mpango wa kutoa elimu kuhusu ugonjwa huo hata kwa shule za msingi.Japokuwa watoto kutoka familia zilizo na pato la chini ndio wanaothirika zaidi kutoka na ukosefu wa lishe bora serikali imejikakamua kuhakikisha inatoa matibabu ya bure kwa kila mmoja.

Mtaalam mmoja wa maswala ya kiafya katika chuo kikuu cha Botswana Narain Sinha anasema ukosefu wa elimu miongoni mwa wanawake miongoni na maswala mengine huenda likaendelea hata kusababisha matatizo zaidi katika ongezo la watoto wanaofariki jambo asilokubaliano nalo Bi Fatma.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2001 iliyotolewa na umoja wa mataifa asilimia 38.5 ya watu walio kati ya umri wa miaka 15-49 walikuwa wameambukizwa virusi vya hiv. Wizara ya afya nchini Botswana ina imani kuwa taifa hilo litafanikiwa kutimiza lengo hilo la nne la maendeleo ya milenia la umoja wa mataifa, la kupunguza idadi ya vifo vya watoto kwa thuluthi mbili kufikia mwaka 2015. Serikali kwa sasa imelipa kipaumbele swala la vifo va watoto wachanga.