1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifo vya raia vyaongezeka Iraq.

1 Aprili 2008
https://p.dw.com/p/DYqe

Baghdad.

Serikali ya Iraq imesema kuwa vifo vya raia vinavyotokana na ghasia nchini humo vimeongezeka na kufikia katika kiwango cha juu kabisa tangu katikati ya 2007.

Idadi ya raia waliouwawa March imepanda hadi kufikia watu 923, kutokana na ongezeko la ghasia zinazosababishwa na mapigano kati ya wanamgambo wa Kishia na majeshi ya usalama ya Iraq.

Waziri mkuu Nuri al-Maliki leo amedai kuwa mapambano na wanamgambo wa Kishia mjini Basra yamefanikiwa na yamesaidia kuweka utawala wa sheria katika mji huo wa pili kwa ukubwa nchini humo.

Wakati huo huo watu wenye silaha wamewapiga risasi polisi sita wa kikabila karibu na mji wa Tikrit, kaskazini mwa Baghdad. Vikundi hivyo vya polisi vinapatiwa fedha na Marekani na vimeundwa katika maeneo ya Wasunni nchini Iraq kupambana na wapiganaji kutoka katika kundi la kigaidi la Al-Qaeda.