1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifo vya corona vyapindukia nusu milioni duniani

29 Juni 2020

Zaidi ya watu nusu milioni wamefariki duniani kutokana na ugonjwa wa virusi vya corona, huku karibu theluthi mbili wakiwa nchini Marekani na Ulaya, kwa mujibu wa hesabu zilizowekwa pamoja na shirika la habari la AFP.

https://p.dw.com/p/3eUWx
Brasilien Coronavirus Protestaktion in Rio de Janeiro
Picha: Getty Images/B. Mendes

Idadi rasmi ya vifo kutokana na ugonjwa huo wa covid-19 imefikia 500,390 kutokana na jumla ya visa 10,099,576 vilivyorikodiwa kote duniani. Marekani inaongoza kwa kuwa na vifo 125, 747, ikifuatiwa na Brazil yenye vifo 57,622 na Uingereza inashika nafasi ya tatu kwa kurekodi vifo 43,550. Lakini takwimu hizo zilizokusanywa kutoka kwa mamlaka za kitaifa na taarifa za shirika la afya duniani WHO, yumkini zinaakisi sehemu ndogo tu ya idadi halisi ya maambukizi, kutokana na ukweli kwamba mataifa mengi yanapima tu visa vikali zaidi vya maambukizi hayo.