1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA:Wakaguzi wa IAEA Kuelekea Korea kaskazini baada ya kupata idhini

11 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBk0

Wakaguzi wa kimataifa wanajiandaa kwenda Korea kaskazini baada ya nchi hiyo kutoa rasmi idhini ya wakaguzi hao kuingia.

Bodi ya magavana wa shirika la kimataifa la kudhibiti technologia ya Nuklia IAEA imekubali mwaliko huo.

Hii ni mara ya kwanza kwa wakaguzi wa shirika hilo kuingia Korea kaskazini tangu mwaka 2002.

Wakaguzi hao watawajibika kuhakikisha hatua za mwanzo za kuharibu mpango wa kutengeneza sialaha za Nuklia wa Pyongyang.Hatua hiyo inatazamiwa kuwa ngumu na itakayochukua muda mrefu.