1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA.Mpatanishi wa nyuklia wa Iran kukutana na El Baradei

9 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTi

Mpatanisha mkuu wa mpango wa nyuklia wa Iran Ali Larijani atakutana na mkurugenzi wa shirika la kimataifa linalothibiti nishati ya atomiki Mohamed Al Baradei katika mji mkuu wa Vienna, nchini Austria.

Bwana Larijani yuko njiani kuelekea katika mkutano wa 43 wa usalama wa kimataifa utakao fanyika mini Munich hapa nchini ujerumani.

Atakapokuwa hapa nchini Larijani atakutana pia na kansela wa Ujerumani Angela Merkel na mkuu wa sera za nje wa umoja wa ulaya Javier Solana kujadili mzozo wa nyuklia wa Iran kandoni mwa kongamano hilo la usalama.