1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA : Waziri Mkuu wa Italia akutana na Larijani

9 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDEA

Waziri Mkuu wa Italia Romano Prodi amekutana na msuluhishi mkuu wa suala la nuklea wa Iran Ali Larijani na kumtaka kutanzua kikwazo cha kidiplomasia juu ya mpango wa nuklea wa serikali ya Iran.

Mkuu wa masuala ya sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Javier Solana amefuta uwezekano wa kuwekewa vikwazo Iran kwa kadri mazungumzo na nchi hiyo yatakapokuwa yanaendelea.Solana anatazamiwa kukutana na Larijani leo hii mjini Vienna.

Marekani inasema inataka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuanza mazungumzo wiki ijayo juu ya rasimu ya azmio ambalo litaweka vikwazo dhidi ya Iran kutokana na shughuli zake za nuklea.

Msaidizi waziri wa mambo ya nje wa Marekani Nicholas Burns amesema vikwazo hivyo viilenge serikali na mitambo yake ya nuklea na sio wananchi wa Iran.