1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA: Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa kwenda Korea Kaskazini Jumamosi ijayo

11 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjw

Wachunguzi wa shirika la kimataifa la kuzuia utapakazaji wa silaha za kinyuklia, IAEA, wanatarajiwa kuwasili nchini Korea Kaskazini Jumamosi ijayo kusimamia kutimizwa kwa ahadi ya kukifunga kinu cha nyuklia cha Yongbyon.

Hii leo kiongozi wa shirika hilo, Mohamed El Baradei, amesema Korea Kaskazini inaonekana inajiandaa kukifunga kinu cha Yongbyon kama sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa mwezi Februari mwaka huu kwenye mkutano wa mataifa sita mjini Beijing China uliozungumzia mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Makubaliano hayo yaliyofikiwa baina ya Korea Kaskanzini, Korea Kusini, China, Japan, Urusi na Marekani, yanairuhusu Korea Kaskzini kupokea tani 50,000 za mafuta kutoka Korea Kusini.

Shehena ya kwanza ya mafuta hayo inatazamiwa kuwasili Jumamosi ijayo.