VIENNA : Umoja wa Ulaya yataka Iran irepotiwe kwa mpango wake wa nuklea
24 Septemba 2005Matangazo
Umoja wa Ulaya umewasilisha azimio kwa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomu IAEA ambalo linaweza kuifikisha Iran kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa uwezekano wa kuwekewa vikwazo kutokana na mpango wake nuklea.
Rasimu ya azimio hilo linalitaka shirika hilo la IAEA kuiripoti Iran kwa sababu ya kuwepo kwa hofu kwamba taifa hilo la Kiislam linaendesha mpango wa siri wa kutengeneza silaha za nuklea.Russia, China na nchi kadhaa kwenye bodi ya shirika hilo zimepinga hoja hiyo.
Bodi ya IAEA inatazamiwa kukutana tena leo hii kufikiria pendekezo hilo.