1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA: Ukuzaji wa bangi waongezeka Afghanistan

26 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBoG

Kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na madawa ya kulevya na uhalifu, UNODC, ukuzaji bangi nchini Afghanistan uliongezeka kwa aislimia 50 mwaka jana.

Ripoti hiyo inasema Afghanistan inazalisha asilimia 90 ya bangi duniani, licha ya juhudi za kuyaharibu mashamba ya bangi nchini humo kuungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.

Lakini ripoti hiyo pia inataja eneo la Golden Triangle huko Asia Kusini ambalo lilikuwa mtoaji mkubwa wa dawa ya kulevya ya heroin kama mfano mzuri wa ufanisi. Inasema eneo hilo sasa linakaribia kuwa huru kutokana na bangi kufuatia juhudi kubwa za kuzuia kilimo cha bangi.