VIENNA: Shirika la IAEA laljiandaa kutoa ripoti kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran
22 Februari 2007Shirika la umoja wa Mataifa la kuzuia usambazaji wa silaha za kinyuklia, IAEA, linajiandaa kutoa ripoti mbayo huenda ikalifungulia mlango baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, kupanau vikwazo vyake dhidi ya Iran kuhusina na mpango wake wa nyuklia.
Duru katika shirika hilo mjini Vienna nchini Austria zinasema ripoti hiyo huenda ikaishtaki Iran kwa kuongeza shughuli zake za mpango wake wa nyuklia badala ya kuzipunguza kama ilivyotakikana na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Baraza hilo liliiwekea Iran vikwazo miezi miwili iliyopita kwa kukataa kusitisha shuhguli zake za kurutubisha uranium.
Mataifa mengi ya maghairibi yanahofu Iran huenda inapania kutengeneza silaha za kinyuklia lakini Iran imeendelea kupinga huku ikisisitiza mpango wake huo ni wa matumizi ya amani.