1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vienna. Ripoti ya baraza la Congress inapotosha.

15 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDCE

Shirika la umoja wa mataifa la kudhibiti teknolojia ya kinuklia limeilaumu serikali ya Marekani kuhusiana na ripoti ya baraza la Congress ambayo inadokeza kuwa mpango wa kinuklia wa Iran umepiga hatua zaidi kuliko unavyoelezwa na wachunguzi wa umoja wa mataifa.

Shirika la kimataifa la tekonolojia ya kinuklia limeieleza ripoti hiyo ya baraza la Congress kuwa isiyo na ukweli na inayovuka mipaka. Katika barua ya malalamiko kwa serikali ya Marekani , maafisa wa umoja wa mataifa wamesema kuwa maafisa wa kijasusi wa Marekani wamekosea wanaposema kuwa Iran imerutubisha madini ya Urani na kufikia kiwango cha kutengeneza silaha wakati ukweli ni kuwa shirika la IAEA limegundua tu kiwango kidogo cha ambacho kiko katika kiwango cha chini mno.

Wachunguzi wa umoja wa mataifa wamekuwa wakichunguza mpango wa kinuklia wa Iran tangu mwaka 2003 na hadi sasa hawajagundua ushahidi unaotoa ishara kuwa Iran inatengeneza silaha za kinuklia.