1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA: Putin azuru Austria

23 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzJ

Rais wa Urusi, Vladamir Putin, anatarajiwa kuwasili hii leo nchini Austria katika ziara yake ya kwanza ya kigeni tangu Urusi kufanya mkutano na Umoja wa Ulaya uliotuwama juu ya uhuru wa kidemokrasia.

Rais Putin anafanya ziara hiyo kwa lengo la kuboresha biashara baina ya Urusi na Austria, nchi inayoonekana kama daraja ya kiuchumi baina ya nchi za mashariki na magharibi.

Mikataba 20 inatarajiwa kusainiwa, hasa katika sekta ya nishati na utengenezaji wa magari. Lakini rais Putin huenda akakakosolewa vikali kwa historia ya Urusi kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu wakati atakapokutana na rais wa Austria, Heinz Fischer na kansela Alfred Gusenbauer.

Mkutano baina ya Urusi na Umoja wa Ulaya wiki iliyopita ulimalizika na mabishano makali kuhusu demokrasia.