1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vienna: Mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomiki...

26 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFp2

Mohammed Al Baradei anatazamiwa kufika ziarani mjini Tripoli kesho kwa lengo la kuchunguza kwa kina mipango ya kinuklea ya Libya.Ziara hiyo imesadif wiki moja tuu baada ya Libya kutangaza nia ya kuachana na mipango ya kutengeneza silaha za maangamizi.Uamuzi huo umepitishwa baada ya miezi tisaa ya mazungumzo ya siri kati ya Libya,Uengereza na Marekani.
Msemaji wa shirika hilo la kimataifa Mark GWOZDECKY amesema ziara hiyo imelengwa kuanzisha utaratibu wa kuchunguzwa kwa kina harakati zote za kinuklea za Libya,za kale na za sasa .Serikali ya kanali Muammar Gaddafi imeahidi pia kuidhinisha itifaki ziada ya makubaliano ya kutosambaza silaha za kinuklea.