1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA : Mataifa makuu ya Ulaya yarasimu azimio dhidi ya Iran

19 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEZi

Mataifa makuu matatu ya Umoja wa Ulaya yameanza kurasimu azimio lenye kuitaka shirika la nuklea la Umoja wa Mataifa kuirepoti serikali ya Iran kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuangalia uwezekano wa kuwekewa vikwazo.

Rais Mahmoud Ahamedinejad wa Iran ameliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapo Jumamosi kwamba serikali yake imenuwia kuendelea kuzalisha nishati ya nuklea.Mataifa ya magharibi yamekuwa yakihofia kwamba mpango wa nuklea wa Iran unaweza kutumika kutengeneza silaha za nuklea.

Ikiwa imevunjwa moyo na msimamo huo wa Iran Ujerumani,Ufaransa na Uingereza zimeamuwa kuliomba Shirika la Nishati ya Atomiki la Umoja wa Mataifa IAEA kuifikisha Iran kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kufikiria kuiwekea vikwazo vya kiuchumi.

Shirika hilo la IAEA litajadili suala hilo wakati wa mkutano wa wiki moja unaoanza leo hii.