1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA: Iran yatuhumiwa haishirikiani na IAEA

8 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLJ

Iran imetuhumiwa na Umoja wa Ulaya kwa kukosa kushirikiana na Shirika la Nishati ya Atomu la Umoja wa Mataifa,IAEA.Katika taarifa iliyotolewa kwenye mkutano wa bodi ya IAEA mjini Vienna,Ujerumani,Ufaransa na Uingereza ziliikosoa Iran kwa kutaka kuongeza harakati za kurutubisha uranium kwa kiwango cha kuweza kuzalisha nishati ya nyuklia.Kwa upande mwingine mjini New York, wanachama watano wenye viti vya kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani pia,wamekuwa na majadiliano yenye lengo la kuongeza vikwazo vilivyo idhinishwa mwisho wa mwaka jana dhidi ya Iran.Marekani na Umoja wa Ulaya zina hofu kwamba Iran huenda ikawa inajaribu kutengeneza silaha za kinyuklia.Iran imekanusha madai hayo na inasema mradi wake wa nyuklia ni kwa matumizi ya amani tu.