1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA: Iran yatishia kuanza kurutubisha madini ya uranium

18 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEZn

Mataifa matatu ya umoja wa Ulaya, Ujerumani, Uingereza na Ufaransa, yakiwa yamechoshwa na mwenendo wa Iran wa kutaka kuendelea kutengeneza silaha za nyuklia, yameanza kutayarisha azimio la kulitaka shirika la kimataifa la nishati ya atomiki, kuishitaki Iran mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Iran nayo kwa upande wake imesema itaanza tena kuyarutubisha madini ya uranium ikiwa shirika hilo la kimataifa litachukua hatua hiyo.

Uwezekano wa Iran kufikishwa mbele ya baraza hilo uliongezeka wakati rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad alipohutubia katika mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa mjini New York, Marekani.

Kiongozi huyo alisisitiza kwamba nchi yake ina haki ya kuendelea mbele na mpango wake wa nyuklia na kwamba Marekani haina haki yoyote ya kuuzuia mpango huo wa Iran, kwani Marekani ndilo taifa pekee ambalo limewahi kutumia silaha za nyuklia.