1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Verstappen aibuka mshindi Saudi Arabia Grand Prix

28 Machi 2022

Kinyang'anyiro cha ubingwa wa dunia mwaka wa 2021 kilikuwa kikali mwaka mzima kabla ya Max Verstappen kumpiku kwa njia ya utata Lewis Hamilton na kubeba taji hilo kwenye mzunguko wa mwisho wa mbio za kuumaliza msimu.

https://p.dw.com/p/498d2
Formel 1 | GP Saudi-Arabien | Max Verstappen
Picha: Hassan Ammar/AP/picture alliance

Katika mbio za magari ya Formula One, kinyang'anyiro cha ubingwa wa dunia mwaka wa 2021 kilikuwa kikali mwaka mzima kabla ya Max Verstappen kumpiku kwa njia ya utata Lewis Hamilton na kubeba taji hilo kwenye mzunguko wa mwisho wa mbio za kuumaliza msimu.

Na msimu mpya wa 2022 ukiwa umeshuhudia mikondo miwili tu, kuna kila aina ya ishara ya kuwepo uhasama na ushindani wenye kila aina ya visa na vituko vinasubiri kati ya dereva wa timu ya Red Bull Verstappen na wa Ferrari Charles Leclerc.

Baada ya Ferrari kushinda mbio za Bahrain Grand Prix kwa Leclerc na Carlos Sainz kumaliza nafasi mbili za kwanza, Verstappen alirejea kwa kishindo jana katika mbio za Saudi Arabia Grand Prix na kushinda mbele ya Leclerc na Sainz. Leclerc ana pointi 43 dhidi ya Verstappen ambaye ana 25 wakati madereva hao wakijiandaa kuelekea Melbourne Australia katika wiki mbili zijazo.

afp