VATICAN.Vatikani mbioni kutuliza hamasa za waislamu
19 Septemba 2006Kufuatia kuongezeka kwa wimbi la kukosolewa kwa hotuba ya Baba mtakatifu Benedikti wa 16 makao makuu ya kanisa katoliki Duniani Vatikani yamelazimika kuchukua hatua zaidi kutuliza hasira za waislamu.
Licha ya kiongozi huyo wa kidini kuomba msamaha,Vatikani imewaamuru wajumbe wake katika mataifa ya kiislamu kufafanua matamshi ya baba mtakatifu katika hotuba yake juu ya Uislamu.
Nchini Iraq hata hivyo kundi la al Qaeda limesema kwenye taarifa yake katika mtandao kwamba litalivunja kanisa katoliki.
Mamia ya watu pia wameandamana mjini Basra huko Ira na kuchoma kinyago cha mtakatifu huyo wa kanisa katoliki duniani.
Wimbi hili la hasira katika ulimwengu wa kiislamu limezuka baada ya kiongozi huyo wa kikatoliki kumnukulu mfalme wa karne ya 14 Byzantine aliyesema baadhi ya mafunzo ya mtume Mohammad S.A.W yalikuwa maouvu na yasiyo ya kiutu.