1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATICAN: Hotuba ya papa haikulenga kuwaudhi waislamu

15 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDC7

Makao makuu ya kanisa Katoliki, Vatican, yamesema hotuba ya Baba Mtakatifu haikulenga kuwaudhi waislamu. Viongozi wa kiislamu wameikosoa vikali hotuba ya kiongozi wa kanisa Katoliki Baba Mtakatifu Benedict wa 16, alipozungumzia kuhusu vita vitakatifu vya jihad.

Akizungumza wakati wa ziara yake hapa Ujerumani, papa Benedict wa 16 alimnukulu mfalme wa kikristo wa karne ya 14, Manuel II, aliyesema kwamba mtume Muhammad ameleta tu mambo mauovu na yasiyo na ubinadamu.

Kiongozi wa baraza la waislamu, Muslim Brotherhood, amesema matamshi ya papa yamezusha hasira kubwa miongoni mwa jamii ya waislamu duniani kote.

Hotuba yake pia ilitaka msamaha kutoka kwa kiongozi wa kidini nchini Uturuki, ambako papa Benedict wa 16 atazuru mwezi Novemba mwaka huu katika zaira yake ya kwanza ya taifa la kiislamu.