1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VALENCIA : Wanasayansi waandaa repoti ya hali ya hewa

12 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBJh

Wanasayansi waandamizi wa Umoja wa Mataifa wanakutana katika mji wa Valencia nchini Uhispania leo hii kuanza kuandaa repoti ya mwisho kati ya repoti nne mwaka huu juu ya kuongezeka kwa kiwango cha ujoto duniani.

Waraka huo wa kurasa 10 na Jopo la Kiserikali juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa IPCC utajumuisha ukubwa na athari za ongezeko la ujoto na kile kinachoweza kufanywa na serikali kuzuwiya ongezeko la ujoto duniani kunakosababishwa na utowaji wa gesi zenye kuathiri mazingira.

Repoti hiyo inatowa msingi wa kisayansi kwa ajili ya mkutano wa Umoja wa Mataifa uliopangwa kufanyika mjini Bali Indonesia mwezi ujao.Repoti ya jopo hilo inatazamiwa kutolewa hapo Jumamosi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban- Ki moon.

Jopo la IPCC ni washindi wenza wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka huu.