VALENCIA: Mabadiliko ya hali ya hewa yaathiri zaidi nchi masikini
13 Novemba 2007Matangazo
Wataalamu wa kisayansi na wajumbe wa jopo la Kiserikali juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa IPCC kutoka nchi 145 wanakutana Valencia nchini Uhispania.Wataalamu hao wanashauriana njia za kupambana na tatizo la ongezeko la ujoto duniani.
Katibu Mtendaji wa IPCC,Yvo de Boer amesema, athari za mabadiliko ya hali ya hewa zimedhihirika.Akaongezea kuwa nchi masikini ndio zitaathirika vibaya zaidi na hata uhai wa baadhi ya watu upo hatarini.