VALENCIA : Kupuuza hali ya hewa ni kutenda uhalifu
12 Novemba 2007Matangazo
Afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa juu ya hali ya hewa leo ametowa changamoto kwa wanasiasa na wabunge duniani kuandaa mpango wa kuzuwiya mabadiliko ya hali ya hewa na kwamba kupuuza muhimu wa suala hilo kutakuwa sawa na kutenda uhalifu.
Yvo de Boer mkurugenzi wa Mpango wa Makubaliano ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa wa Umoja wa Mataifa alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa wanasayansi waandamizi wa Umoja wa Mataifa katika mji wa Valencia nchini Uhispania leo hii kuanza kuandaa repoti ya mwisho kati ya repoti nne mwaka huu juu ya kuongezeka kwa kiwango cha ujoto duniani.
De Boer amesema ongezeko la ujoto duniani litaathiri zaidi nchi za kimaskini na kutishia kuendelea kuishi kwa baadhi ya watu.