Uwezekano wa uasi nchini Mali
18 Agosti 2020Ubalozi huo umesema umefahamishwa kuhusu uasi huo katika jeshi la Mali na vikosi vimo njiani kuelekea Bamako.
Ubalozi huo wa Norway umesema katika taarifa ya tahadhari kwa raia wao kwamba raia wa Norway wanapaswa kuchukua tahadhari na kubakia majumbani mwao hadi hali hiyo itakapotulia.
Chanzo cha usalama kimesema ni kweli kuna uasi na wanajeshi wamechukua silaha. Msemaji wa jeshi alithibitisha kuwa milio ya risasi ilisikika katika kituo cha jeshi cha Kati, kiasi ya kilometa 15 nje ya mji mkuu Bamako, lakini alisema hana taarifa zaidi.
Uasi katika kituo cha jeshi cha Kati umesababisha mapinduzi ya mwaka 2012 ambayo yaliuondoa utawala wa Rais Amadou Toumani Toure na kuchangia eneo la kaskazini nchini Mali kuangukia mikononi mwa wapiganaji wa Jihadi.
(Reuters)