1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki yaongeza kodi kwa bidhaa za Marekani

15 Agosti 2018

Tofauti zaa kidiplomasia kati ya Uturuki na Marekani inazidi kushika kasi baada ya mahakama moja nchini Uturuki kukataa ombi la kumuondolea kizuizi cha nyumbani na marufuku ya kusafiri kasisi mmarekani  Andrew Brunson.

https://p.dw.com/p/33C1L
US-Produkte Made in America
Picha: Reuters/F. Bensch

Hayo yatatokea katika kipindi ambapo serikali ya Uturuki  imetangaza kuongeza viwango vipya vya kodi kwa baadhi ya bidhaa za Marekani zinazoingizwa nchini humo.

Lakini pamoja na hatua hiyo dhidi ya mchungaji huyo raia wa Marekani,  anayetajwa kuwa na mahusiano na kiongozi wa kidini anayeishi Marekani, ambaye anatuhumiwa kuhusika na jaribio lililoshindwa la mapinduzi nchini Uturuki la mwaka 2016, mwanasheria wake aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba, mahakama ya juu bado haijtatoa uamuzi wake kuhusu rufani ya kesi hiyo.

Mchungaji huyo wa Kiinjilisti Andrew Brunson anashitakiwa nchini Uturuki kwa tuhuma za ugaidi. Na kesi yake hiyo kwa sasa inatajwa kuwa ni kitovu cha mgogoro wa kidiplomasia kati ya Uturuki na Marekani, jambo ambalo limechangia kuporomoka kwa thamani ya sarafu ya Uturuki.

Maeno ya nyongeza ya kodi kwa Marekani

Türkei | Proteste gegen US-Sanktionen
Waandamanaji Uturuki wakipinga vikwazo vya MarekaniPicha: picture-alliance/AA/D. Keskinkilic

Kwa muendelezo ya tofauti hiyo Uturuki tayari imetangaza kuongeza tozo la  viwango vya kodi kwenye bidhaa kadhaa muhimu za Marekani, na katika kile kinachoonekana kama hatua ya kulipiza kisasi baada ya vikwazo vya Marekani kwa taifa hilo, ambalo athari zake zimeanza kujitokeza kwa kuanza kuporomoka na kutokuwepo kwa ishara yoyote kumalizika kwa hali hiyo. Sarafu hiyo imepoteza thamani ya karibu robo ya nguvu yake jambo linalotishia kulingiza taifa hilo katika mgogoro wa kiuchumi.

Mkazi wa Ajnkara Serkan Kadroglu alisema "Kwa sasa viwango vya kubadilisha fedha ya ndani ni vya chini sana, kwa hivyo sitaki kubadili pesa. Lakini kupanda kwa thamani ya fedha za kigeni sio jambo zuri hata kidogo kwa uchumi wa taifa."

Makamu wa Rais wa Uturuki Fuat Oktay amesema nyongeza ya ushuru imewekwa kwa kuziungatia mfumo wa kufanikisha usawa  wa kibiashara ikiwa ni majibu kutokana na shambulio la utawala wa Marekani kwa uchumi wa taifa lao. Bidhaa ambazo zinatajwa katika nyongeza ya kodi ambazo zinaingizwa nchini Uturuki ni pamoja na mchele, magari, vileo, makaa ya mawe na bidhaa za mapambo. Maeneo mengine ni kwenye magari ya Kimarekani ambayo kodi yake imeongezwa mara mbili zaidi hadi asilimia 120 wakati kodi kwenye vinywaji vya pombe ikiongezwa na kufikia asilimia 140.

Hivi karibuni Rais wa Marekani alitangaza kuongeza maradufu kwa ushuru wa bidhaa za Uturuki za chuma na bati, kiini cha tofauti hiyo kwa mataifa hayo mawili washirika katika umoja wa kujihami wa NATO ni hicho kitendo cha serikali ya Uturuki kumweka kizuizini mchungaji wa Andrwe Brunson.

Hapo jana Rais wa Uturuki Racep Tayyip Erdogan alisema taifa lake litachukua hatua ya kugomea ununuzi wa bidhaa za kieletroniki kutoka Marekani simu ya mkononi aina ya  iPhone, pomoja na yeye mwenyewe kuelezwa kujipiga picha mara kadhaa kwa kutumia aina hiyo ya simu. Pia aliwahi kutoa hotuba maarufu sana usiku wa Julai 2016 wakati wa jaribio la mapinduzi lililoshindwa kwa kutumia program ya iPhone iitwayo FaceTime, akiwataka wananchi watoke mitaani kupinga hatua hiyo.

Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman