1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Ugaidi

Uturuki yafanya mashambulizi mengine dhidi ya wakurdi Iraq

5 Oktoba 2023

Uturuki imesema vikosi vyake vya anga vimefanya mashambulio na kuharibu maeneo 58 kaskazini ya Iraq yanayoshikiliwa na chama kilichopigwa marufuku cha wafanyakazi wa Kurdistan (PKK).

https://p.dw.com/p/4X9Lx
Türkiische Streitkräfte führen Operation gegen PKK nahe der irakischen Grenze durch
Picha: Ozkan Bilgin/AA/picture alliance

Uturuki imesema vikosi vyake vya anga vimefanya mashambulio na kuharibu  maeneo 58 kaskazini ya Iraq yanayoshikiliwa na chama kilichopigwa marufuku cha wafanyakazi wa Kurdistan (PKK) kundi lililodai kuhusika na shambulio la bomu la Jumapili iliyopita kwenye wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo mjini Ankara.

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki, Hakan Fidan amefahamisha kuwa vikosi vya nchi hiyo vimefanya mashambulio hayo ya anga kulipiza kisasi na kwamba serikali yake ina haki ya kuyalenga maeneo na nyenzo za makundi ya Wakurdi ya PKK nchini Iraq na kundi la YPG la nchini Syria.

Hata hivyo wakurdi wa nchini Syria wamesema hawahusiki na shambilio hilo la bomu la mjini Ankara na wameeleza kuwa vitendo vya Uturuki ni uhalifu wa kivita.