Uteuzi wa Odinga katika AU una maana gani kuhusu siasa zake?
22 Oktoba 2018Matangazo
Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya, NASA, Raila Odinga ameteuliwa kuwa mwakilishi mwandamizi wa Umoja wa Afrika kwenye masuala ya maendeleo ya miundombinu.
Miongoni mwa majukumu mengi yatakayomkabili, Odinga anataraji kuhamasisha uungwaji mkono wa kisiasa katika masuala ya miundombinu miongoni mwa mataifa wanachama.
Kuhusu uteuzi huu na mengineyo Lilian Mtono amezungumza na mchambuzi wa siasa aliyeko Nairobi Kenya, Profesa Chacha Nyaigoti Chacha, ambaye kwanza anauzungumzia uteuzi huo kwa ujumla.
Mwandishi: Lilian Mtono.
Mhariri:Josephat Charo