Usomaji wa vitabu barani Afrika ni utamaduni ambao haujazoeleka, wengi wakisema kusoma vitabu ni gharama sana. Wanaharakati na wapenzi wa kusoma vitabu wamekuwa na jitihada za kuhakikisha vitabu vinawafikia wananchi kwa bei ndogo. Saumu Mwasimba anaitazama App maalumu nchini Nigeria ya Okadabooks ambayo inawawezesha watu kupakua na kusoma vitabu.