Akaunti za FIFA zafanyiwa uchunguzi
17 Juni 2015Matangazo
Michael Lauber amesema kuwa afisi yake ilikuwa ikichambua idadi kubwa ya data za FIFA zilizopatikana katika uchunguzi wake wa ufisadi katika shirikisho hilo.
Amesema kuwa huenda akamhoji rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter katika mpango wa uchunguzi wake ili kufahamu mengi zaidi kuhusiana na tuhuma hizo za rushwa
FIFA inakabiliwa na tuhuma za ufisadi baada ya maafisa wa polisi wa Uswizi kuivamia hoteli mjini Zurich na kuwakamata maafisa saba wakuu mwezi uliopita.
Maafisa hao saba walikamatwa kufuatia ombi la idara ya mahakama ya Marekani ambayo imewashtaki maafisa 14 wa FIFA wanaohudumu sasa na wale wa zamani pamoja na washirika wao
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Mohamed Khelef