Benki ya Credit Suisse kuomba mkopo wa dola bilioni 54
16 Machi 2023Matangazo
Benki hiyo pia itachukua deni la dola bilioni 2.5 na vilevile italipa deni la Euro milioni 500 ili kurejesha faida kwa wawekezaji. Hisa za benki hiyo zilianguka kwa aslimia 24 hapo jana baada ya kugundulika udhaifu katika taarifa zake za fedha.
Matatizo ya benki hiyo yalijitokeza wiki iliyopita baada ya benki kubwa ya Marekani ya Silicon Valley kusambaratika, pamoja na uamuzi wa mwekezaji mkuu ambaye ni benki ya Saudi Arabia kukataa kuongeza fedha zaidi kwa ajili ya benki hiyo ya Uswisi.
Misukosuko ya benki hiyo imesababisha wasiwasi juu ya mfumo wa fedha barani Ulaya kama mgogoro mkubwa wa mabenki uliotokea mnamo mwaka 2008.