Usman dan Fodio: Mwanzilishi wa Ukhalifa wa Sokoto
Historia
Yusra Buwayhid
11 Februari 2020
Usman dan Fodio amezaliwa katika familia ya walowezi wa awali wa kabila la Fulani waliohamia eneo la watu wanaozungmuza Kihausa tangu karne ya 15. Alikuwa ni mwalimu mashuhuri wa dini ya Kiislam. Alitumia mitazamo yake ya kidini kuwahamasisha wafuasi wake kuunda kundi la kijeshi, na kupigana vita vya kidini dhidi ya viongozi wa Kihausa kuanzia mwaka 1804.