MigogoroJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Usitishaji mapigano mashariki mwa Kongo waafikiwa
31 Julai 2024Matangazo
Hayo yametangazwa na ofisi ya rais wa Angola, nchi hayo ambayo imekuwa mpatanishi katika duru kadhaa za mazungumzo ya kumaliza uhasama kati ya Kongo na Rwanda kuhusiana na vita vinavyoendelea mashariki mwa Kongo.
Serikali ya Kongo imekuwa ikiituhumu Rwanda kuwaunga mkono waasi wa M23 wanaoendesha hujuma mashariki mwa Kongo.
Kulingana na ofisi ya rais Joao Lourenco wa Angola, usitishaji mapigano utaanza usiku wa manane wa Agosti 4 na utaratibu utawekwa kusimamia utekelezaji wake.
Makubaliano hayo yamepatikana wakati wa mkutano wa mawaziri wa kigeni wa mataifa hayo mawili ulofanyika katika mji mkuu wa Angola, Luanda. Yameafikiwa wakati makubaliano mengine ya kusitisha mapigano chini ya misingi ya kiutu yanaelekea kufikia mwisho mnamo Agosti 3.