1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ushawishi wa Obama katika mkutano wa mazingira bonn.

8 Aprili 2009

Kwa kadiri gani kurejea kwa Marekani katika mjadala wa kulinda mazingira kutachangia mapatano Copenhagen ?

https://p.dw.com/p/HT1t
Chancellor Angela Merkel na Barack Obama.Picha: AP

Duru ya kwanza kabla ya mkutano ujao wa ulimwengu juu ya mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa mjini Copenhagen,Denmark imemalizika. Majadiliano juu ya mkataba mpya wa mazingira ulimwenguni yamemalizika mjini Bonn,Ujerumani.Na ingawa hakuhudhuria binafsi,ushawishi wa Rais Obama ,ulibainika wazi katika majadiliano ya Bonn.Na ingawa kuna bado duru 2 kubwa kabla mkataba mpya unaofuatia ule wa Kyoto, kuidhinishwa mjini Copenhagen,na viongozi wa kimataifa hapo Desemba,majadiliano ya Bonn na ushjawishi wa Obama, tayari unaleta matumaini mema:

Majadiliano yalioingiza wajumbe kutoka nchi 175 mbali mbali yalichukua siku 11 mjini Bonn.Licha ya kuwa ,kwa kadiri kubwa , hali njema ya hali ya hewa ilitanda mjini Bonn ,kwa wajumbe kiasi cha 2.600, matarajio kutoka mkutano huo hayakuwa mazuri.

Kwani linapokuja swali la kujitwika jukumu maalumu hasa nchi za kiviwanda zilizokumbwa na msukosuko wa kiuchumi wakati huu,wajumbe wake wengi ,wakitaka kuuliza nyumbani iwapo nchi zao zamudu kugharimia.

Miradi ya kuutia jeki uchumi na kuyaokoa mabenki mashirika ya bima na viwanda visifilisike,kunaufanya msukosuko wa mabadiliko ya hali ya hewa kupewa kisogo kwa sasa au kwa kipindi kijacho cha uchaguzi.

Katika hali kama hiyo, ilikuwa kuvuta pumnzi kusikia risala ya mjumbe wa Marekani mwanzoni mwa majadiliano haya mjini Bonn.

Ingawa hakutoa ahadi madhubuti lakini kama rais wake Barack Obama wakati wa ziara yake ya hivi punde barani Ulaya,mjumbe huyo wa Marekani ameeneza mjini bonn matumaini na moyi mwema.Jinsi alivyotoa matumaini hayo, wajumbe walisimamya kumshangiria.

Hatahivyo, ushawishi hapa wa Obama haukudhihirika wazi.Si wajumbe wa serikali,si wachunguzi wala mashirika yasio ya kiserikali ,wote walimfurahia mkuu wa Shirika la mazingira la UM Yvo de Boer,aliposema kuwa Marekani sasa imejiunga tena na safari ya kulinda mazingira.Marekani haikutoa ahadi madhubuti itafanya nini mbali na kwamba Rais wa marekani ameahidi kuwa Marekani hadi ifikapo 2020 itapunguza moshi unapaa angani kuchafua mazingira katika kiwango cha 1990.

Bila shaka hii haitoshi,hatahivyo wajumbe wengi mkutanoni walikumbuka ilivyokua mjini Bali,2007 pale Marekani ilipokataa katakata kuidhinisha mapatano ya Kyoto na juu ya hivyo,ikaiitia munda mipango kadhaa.

hatahivyo, kila mmoja anaelewa kwamba bila ya ushirikiano wa mataifa yanayochafua mno mazingira,haitawezekana kuepusha kuchafuka zaidi kwa mazingira na hali ya hewa.Hata Rais anaependwa ulimwenguni kama Barack Obama anabidi nyumbani kuhalalisha hatua zake na hasa kuidhinisha mapatano yaliokubaliwa.

Kwa ufupi, kutoka majadiliano yaliofanyika a Bonn, kuna matumaini ya kusitasita.Inahitajika pia katika mtandao wa Shirika la mazingira la UM arkabu za saa kuendelea kuonesha : zimesalia siku 241 kutoka leo kabla mkutano wa Copenhagen ambako itaamuliwa sisi binadamu tutajikaba roho wenyewe na kutoweza kuvuta pumzi kwa kuchafua hali ya hewa.