Ushahidi wa vidio kutumika CHAN 2018
12 Januari 2018Mfumo huo unaruhusu maafisa walioko nje ya uwanja kusaidia waamuzi katika mchezo katika masuala kama linalooingia goli, mikwaju ya penalti, kadi nyekundu na inapotokea mchezaji ameadhibiwa kwa makosa.
Mfumo huo umetumika katika ligi ya Italia Serie A na Bundesliga nchini Ujerumani msimu na unaanza kutumika kwa mara ya kwanza pia katika ligi ya Uingereza wiki hii.
Teknolojia hiyo inatarajiwa kuanza kutumika nchini Morocco wakati michezo hiyo itakapofikia robo fainali , ambapo timu zinazoshiriki zinatumia wachezaji wanaocheza ligi za ndani. Timu 16 zinashiriki. Mashindano hayo yalitarajiwa kufanyika nchini Kenya lakini nchi hiyo ilishindwa kutekeleza mashariki ya shirikisho la kandanda barani Afrika CAF na Morocco iliteuliwa kuchukua nafasi hiyo.