1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ushahidi mpya watolewa juu ya mizengwe katika uchaguzi wa Zimbabwe

5 Julai 2008

-

https://p.dw.com/p/EWq4

HARARE

Ushahidi mwingine umefichuliwa juu ya udanganyifu uliofanyika katika uchaguzi wa duru ya pili ya uchaguzi nchini Zimbabwe.Ushahidi huo umerekodiwa katika ukanda wa video na mlinzi mmoja wa gereza Shepherd Yuda ambaye ameshatoroka nchini Zimbabwe.Kwa mujibu wa taarifa zake Yuda ni kwamba watu walikuwa wakisimamiwa na kupewa amri wamchague rais Robert Mugabe.

Wakati huohuo Umoja wa Ulaya umekataa kuutambua ushindi wa rais Mugabe na umetaka uchaguzi mwingine ufanyike haraka iwezekanavyo.Rais Mugabe kwa upande mwingine anaendelea kupinga miito inayotolewa duniani akisema alishinda uchaguzi kihalali.Jana akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake Mugabe mwenye umri wa miaka 84 alifutilia mbali uwezekano wa kufanya mazungumzo na mpinzani wake Mogan Tsvangirai ili kuutatua mzozo wa kisiasa ikiwa Morgan Tsvangirai hatokubali kumtambua kama rais wa Zimbabwe.Upinzani unadai kwamba makundi ya vijana wapiganaji wa rais Mugabe wamewauwa zaidi ya wafuasi wake 100 na kuwakamata wengine kiasi 1500 tangu mwezi Marchi.