SiasaSudan
Usalama wazidi kuzorota nchini Sudan
31 Mei 2023Matangazo
Wapatanishi wa Marekani na Saudi Arabia walisema mnamo siku ya Jumatatu kwamba kikosi cha msaada wa dharura RSF na jeshi wamekubali kurefusha mkataba wa kusitisha mapigano kwa siku tano zaidi. Hata hivyo licha ya tangazo hilo, wakaazi wameripoti kutokea kwa mapigano kusini mwa mji mkuu Khartoum na Nyala ambao ni mji mkuu wa jimbo la Darfur kusini. Jana Jumanne, wakaazi waliliambia shirika la habari la AFP kuwa mashambulizi ya anga na mapigano yaliripotiwa kuendelea hadi nyakati za usiku mjini Khartoum na Darfur. Mkuu wa jeshi Abdel Fattah al- Burham amesema jeshi lake liko tayari kupigana hadi lipate ushindi.