1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Marekani yaonesha uchokozi wa china karibu na Taiwan

Hawa Bihoga
5 Juni 2023

Jeshi la wanamaji la Marekani limetoa video ya kile ilichokiita "maingiliano yasio salama" kwenye mlango wa bahari wa Taiwan, ambapo meli ya kivita ya China ilivuka eneo nyeti la Marekani.

https://p.dw.com/p/4SDHF
USS Chung-Hoon
Picha: Mass Communication Specialist 1st Class Andre T. Richard/U.S. Navy via AP/picture alliance

Maingiliano hayo yanafanyika wakati nchi hizo mbili zikishutumiana kwa kutofanya mazungumzo ya kijeshi, huku kukiwa na hali ya kutoelewana kwa pande zote kuanzia hali ya kibiashara, mzozo wa Taiwan hadi uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Katika video hiyo iliyotolewa najeshi la wanamaji Marekanisiku ya Jumapili, meli ya China imeonekana ikivuka njia ya Chung-Hoon katika maji tulivu ambayo hayabadili mkondo.

Katika video hiyo sauti ilisikika ikituma jumbe wa redio kwa meli ya China, ikionya dhidi ya "majaribio ya kupunguza uhuru wa matumizi ya bahari".

Soma pia:Marekani yasema mazungumzo na china ni muhimu ili kuepuka Mzozo

Hata hivyo, China imetetea hatua yake hiyo na kuishutumu Marekani kwa uchokozi huku ikisisitiza kwamba jeshi lake la maji limechukua hatua madhubuti, salama, halali na za kitaaluma.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Wang Wenbin amewaambia waandishi wa habari kwamba, mara zote China imekuwa ikiheshimu sheria na kanuni za matumizi ya bahari.

"Hatua zinazochukuliwa na jeshi la China ni hatua muhimu za kukabiliana na chokochoko wa baadhi ya nchi."

Ameongeza kwamba China inapinga vikalibaadhi ya nchi kuleta matatizo katika Mlango-Bahari wa Taiwan, na inalinda kwa uthabiti mamlaka yake ya kitaifa na usalama pamoja na amani na utulivu wa kikanda.

China:Tumeonesha ujasiri wetu

Msemaji wa jeshi la China Song Zhongping ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba hatua ya jeshi la wanamaji la China kuzuia ghafla meli ya Marekani ni ishara ya uwezo walionaona ujasiri wa jeshi lao.

China, Peking | Chinesische Regierung protestiert gegen Abschuss ihres Ballons durch die USA
Msemaji wa wizara ya ulinzi China Tan Kefei,Picha: CIS/ROPI/picture alliance

Hii ni mara ya pili katika siku za hivi karibuni kwa China na Marekani kukutana katika mazingira kama haya.

Kulingana na Marekani, mnamo Mei 26, ndege ya kivita ya China ilifanya ujanja wa "uchokozi usio wa lazima" karibu na ndege ya jeshi la Merekani kwenye Bahari ya Kusini ya China katika anga ya kimataifa.

Soma pia:China: Tuko tayari kusambaratisha hatua zozote za kuipatia Taiwan uhuru

Wizara ya ulinzi ya Taiwan siku ya Jumapili ilitaja hatua za China na meli za Marekani na Canada kuwa "uchokozi" na kusema ni jukumu la pamoja la nchi huru na za kidemokrasia kudumisha amani na utulivu katika bahari hiyo.

China inaichukulia Taiwan kama sehemu ya milki yake, madai ambayo serikali ya Taipei imekuwa ikiyapinga kwa nguvu.