1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi:Marekani na Uingereza wanahusika na shambulio Crimea

27 Septemba 2023

Urusi imezituhumu Uingereza na Marekani kuhusika na shambulizi lililofanywa na Ukraine wiki iliyopita dhidi ya Makao Makuu ya Kamandi ya Jeshi ya Majini la Urusi kwenye eneo la Bahari Nyeusi katika rasi ya Crimea.

https://p.dw.com/p/4WswQ
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Urusi Maria Zakharova
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Urusi Maria ZakharovaPicha: Petrov Sergey/Russian Look/IMAGO

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni wa Urusi, Maria Zakharova, amesema Moscow imepata ushahidi usio na mashaka kuwa serikali mjini London na Washington zilikuwa na dhima kwenye shambulizi hilo la Septemba 22. 

Amesema Ukraine ilitumia taarifa za kijasusipamoja na satelaiti za mataifa ya NATO na ndege za ushushushu kupanga na kutekeleza shambulio alilolitaja kuwa "kitendo cha kigaidi".

Soma pia:Ukraine imesema makamada wa jeshi wa Urusi wameuwawa Crimea

Katika taarifa yake mapema wiki hii Ukraine ilisema ilifanikiwa kuwaua makamanda 34 wa jeshi la Urusi na kuharibu kwa sehemu kubwa makao makuu hayo ya kamandi ya jeshi kwenye mji wa Sevastopol, katika rasi ya Crimea iliyonyakuliwa na Moscow tangu mwaka 2014.