1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yawakamata washukiwa wengine mashambulizi ya kigaidi

2 Aprili 2024

Idara ya Usalama ya Urusi (FSB) inawashikilia watu zaidi ambao inawashuku kuhusika na mashambulizi ya kigaidi kwenye ukumbi wa tamasha wa Crocus kaskazini magharibi mwa Moscow zaidi ya wiki moja iliyopita.

https://p.dw.com/p/4eKU6
Ukumbi wa Crocus ulioshambuliwa wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu (IS).
Ukumbi wa Crocus kwenye mkoa wa Moscow, Urusi, ulioshambuliwa wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu (IS).Picha: Maxim Shemetov/REUTERS

FSB ilitangaza siku ya Jumatatu (Aprili 19) kwamba raia wanne wa kigeni, ambao walihusika moja kwa moja katika ufadhili na kuwapa vifaa magaidi, wamezuiliwa mjini Dagestan katika mkoa wa Kaukasi ya Kaskazini.

Vyombo vya habari vya serikali pia vilionesha video iliyotolewa na FSB ambapo mtu mmoja ambaye hakutambulishwa anasema aliwapa silaha wahalifu hao kwenye mji mkuu wa Dagestani, Makhachkala, kufanya mashambulizi hayo katika ukumbi wa Crocus.

Soma zaidi: Watu zaidi wakamatwa kuhusiana na shambulizi la Moscow

Hata hivyo, video hiyo haikuweza kuthibitishwa.

Washukiwa wengi pia walikamatwa nchini Tajikistan.

Kundi la wanamgambo linalojiita Dola la Kiislamu (IS) limedai kuhusika katika mashambulizi hayo ya Machi 22 ambapo idadi ya waliouawa imetajwa kuwa takribani watu 144, huku zaidi ya 550 wengine wakijeruhiwa na baadhi wakiwa bado hawajulikani walipo.