1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yatupilia mbali mazungumzo ya nyuklia na Marekani

2 Oktoba 2024

Urusi imeondoa uwezekano wa mazungumzo ya kuhusu nyuklia na Marekani, ikiangazia msimamo wa Washington kuelekea upanuzi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO.

https://p.dw.com/p/4lLO8
Urusi Moscow | Maria Zakharova
Msemaji wa serikali ya Urusi, Maria Zakharova.Picha: Komsomolskaya Pravda/Russian Look/IMAGO

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, Maria Zakharova, alisema siku ya Jumatano (Oktoba 2) kwamba nchi yake haioni sababu ya mazungumzo na Washington ambayo haiheshimu maslahi muhimu ya Urusi. 

Soma zaidi: Merkel aonya kuhusu kusambaratika kwa siasa za dunia

Zakharova aliongeza kuwa hilo ni tatizo linalotokana na upanuzi wa muungano wa kijeshi wa NATO hadi kwenye mataifa yaliyojiengua kwenye uliokuwa Muungano wa Kisovieti, na linaloibua vitisho dhidi ya usalama wa pamoja.

Siku ya Jumanne, msemaji wa ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov, alisema Urusi isingejadiliana na Marekani juu ya kusaini makubaliano yatakayochukua nafasi ya mkataba wa awali ulioweka ukomo wa silaha za nyuklia kwa mataifa hayo unaomalizika mwaka 2026.