1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yatuma vifaru kusini kukabiliana na Ukraine

10 Agosti 2024

Urusi imetuma vifaru zaidi, makombora na mifumo ya ulinzi upande wa kusini na pia kutangaza hatua za kukabiliana na ugaidi kufuatia uvamizi wa Ukraine kwenye eneo hilo lenye vinu na mitambo ya kusafirishia gesi asilia.

https://p.dw.com/p/4jJaH
Urusi | Kursk
Mashambulizi ya Ukraine katika jimbo la Kursk, kusini mwa Urusi.Picha: MIC Izvestia/IZ.RU/REUTERS

Hayo yanajiri wakati jeshi la Ukraine likisambaza video zinazowaonesha wakiwa wametwaa udhibiti wa mji mmoja mdogo karibu na mpaka, ushahidi wa awali unaothibitisha kusonga mbele kwa jeshi hilo.

Video moja iliyothibitishwa na shirika la habari la Reuters inaonesha msururu wa magari 15 ya jeshi la Urusi yaliyoteketezwa kwa moto kwenye barabara kuu ya mkoa wa Kursk.

Soma: Jeshi la Ukraine laushambulia uwanja wa ndege wa jeshi la Urusi eneo la Lipetsk

Baadhi ya magari hayo yanaonekana yakiwa na maiti za wanajeshi.

Kaimu gavana wa mkoa huo, Alexei Smirnov, amesema mabaki ya droni yameangukia kwenye kituo kidogo cha umeme, karibu na eneo ambalo kuna vinu vikubwa vya nyuklia vya Urusi.