1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi yasema imekidhibiti kijiji kimoja karibu na Bakhmut

Hawa Bihoga
23 Machi 2024

Vikosi vya Urusi vimesema vimekiteka kijiji kimoja kilichopo magharibi mwa mji wa Bakhmut nchini Ukraine, mji ambao Moscow iliudhibiti takriban miezi kumi iliopita katika makabiliano makali na vikosi vya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4e3dY
Mapambano ya kuwania Bakhmut
Mapambano ya kuwania mji wa Ukraine wa Bakhmut yalikuwa makali hadi Urusi ilipotangaza kuudhibiti.Picha: Libkos/AP/picture alliance

Wizara ya Ulinzi ya Urusi katika taarifa yake imesema kuwa kijiji cha Krasnoye katika eneo la Donetsk "kimekombolewa".

Katika wiki za hivi karibuni vikosi hivyo vya Urusi vimedai kuchukua udhibiti wa maeneo kadhaa yalio katika mstari wa mbele wa uwanja wa vita katika wakati  ambao jeshi la Ukraine likabiliwa na uhaba mkubwa wa askari na silaha.

Mwezi uliopita vikosi hivyo viliuteka mji wa kimkakati wa Avdiivka, karibu na mkoa mwingine wa Ukraine unaodhibitiwa na Urusi wa Donetsk, ushindi ambao ulipongezwa na rais wa Urusi Vladimir Putin akisema ushindi huo unaashiria vikosi vyake vimerejea kwenye uwezo wa kufanya mashambulizi.