1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yadungua droni 36 za Ukraine katika Bahari Nyeusi

29 Oktoba 2023

Vikosi vya Urusi vimedungua droni 36 za Ukraine katika anga za Bahari Nyeusi na rasi ya Crimea usiku wa kuamkia leo.

https://p.dw.com/p/4YAJo
Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu akiwa na maafisa wa jeshi la Urusi
Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu akiwa na maafisa wa jeshi la UrusiPicha: Russian Defence Ministry/SNA/IMAGO


Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema jaribio la utawala wa Kyiv kufanya shambulizi la kigaidi kwa kutumia ndege zisizoruka na rubani dhidi ya vituo vilivyoko kwenye mpaka wa Shirikisho la Urusi lilizuiwa. 

Hakuna taarifa yoyote ya haraka kutoka kwa maafisa wa Ukraine kuhusu tukio hilo. Mashambulizi ya Ukrainekwenye mipaka ya Urusi yameongezeka maradufu tangu Kyiv ilipoanzisha operesheni ya kujibu mashambulizi ya Urusi mwezi Juni. 

Soma pia:Urusi: Ukraine yafanya shambulizi karibu na kinu cha nyuklia

Crimea, ambayo ilinyakuliwa na Urusi mwaka wa 2014, aghalabu hulengwa kwa sababu iko karibu na kituo cha Manowari za Urusi katika Bahari Nyeusi na pia barabara muhimu ya usambazaji vifaa kwa askari wa Urusi wanaoyadhibiti maeneo ya kusini na mashariki mwa Ukraine.