1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi haitochunguza ajali ya ndege iliyomuua Prigozhin

30 Agosti 2023

Urusi imeifahamisha mamlaka ya usafiri wa anga ya Brazil kuwa haitoanzisha uchunguzi juu ya ajali ya ndege iliyomuua mkuu wa kundi la mamluki la Wagner Yevgeny Prigozhin chini ya sheria za kimataifa "kwa sasa."

https://p.dw.com/p/4VjIY
Mazishi ya Mkuu wa kundi la Wagner Yevgeny Prigozhin
Mazishi ya Mkuu wa kundi la Wagner Yevgeny Prigozhin Picha: Alexander Zemlianichenko/AP/picture alliance

Yevgeny Prigozhin, manaibu wake wawili na walinzi wanne walikuwa miongoni mwa abiria 10 waliokufa baada ya ndege iliyotengenezwa Brazil aina ya Embraer kuanguka kaskazini mwa mji mkuu wa Moscow wiki iliyopita.

Kituo cha utafiti na usalama wa anga cha Brazil CENIPA, kwa maslahi ya kuboresha usafiri wa anga, kimeeleza utayari wao wa kujiunga na uchunguzi unaoongozwa na Urusi juu ya ajali hiyo, iwapo wangealikwa na uchunguzi huo kufanyika chini ya sheria za kimataifa.

Mkuu huyo wa kundi la mamluki la Wagner amekufa miezi miwili tu baada ya kufanya uasi uliodumu kwa muda mfupi dhidi ya jeshi la Urusi na kutishia utawala wa Rais Vladimir Putin tangu alipoingia madarakani mnamo mwaka 1999.