1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yaripoti milipuko mikubwa baada ya shambulio la droni

8 Julai 2024

Mamlaka ya Urusi imesema Jumapili kwamba shambulizi la droni ya Ukraine lilisababisha milipuko kadhaa katika eneo la kusini mwa Urusi la Voronezh

https://p.dw.com/p/4hzQg
Ukraine Charkiw nach dem russichen Angriff
Picha: Vitalii Hnidyi/REUTERS

Katika ujumbe alioandika kwenye mtandao wa kijamii wa Telegram, gavana wa Voronezh, Alexander Gusev, alisema kuwa vitu vilivyokuwa na nyenzo za kulipuka, vilipuka baada ya droni za Ukraine kudunguliwa karibu na Podgorenski, kusini mwa mji mkuu wa mkoa Voronezh.

Bohari ya kuhifadhi silaha za Urusi yalengwa

Tovuti ya habari ya Ukraine Pravda, iliripoti kuwa bohari ya mita za mraba 9,000 inayohifadhi roketi za jeshi la Urusi, risasi na makombora, ililengwa.

Mamlaka ya Urusi haikuthibitisha ripoti hiyo, lakini kanda za video ziliibuka kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha kufuka kwa moshi mkubwa katika eneo hilo.

Soma pia.Urusi yakisahambulia kwa droni kituo cha nishati cha Sumy

Awali, wizara ya ulinzi ya Urusi haikutoa habari yoyote juu ya shambulio hilo la droni katika eneo la Voronezh, badala yake ilitaja shambulio tofauti la droni za Ukraine katika eneo la mpaka la Belgorod, ambayo inasema lilidunguliwa.