1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yapeperusha bendera yake Crimea

Admin.WagnerD26 Machi 2014

Bendera za Urusi kwa hivi sasa zinapeperushwa katika vituo vya kijeshi mjini Crimea, wakati ambapo Urusi ikiilalamikia Ukraine kwa kukiuka mikataba ya kimataifa ya usafiri wa anga na kuyaweka hatarini maisha ya marubani

https://p.dw.com/p/1BVsa
Ukraine Minensuchboot Donuslaw Versuchter Ausbruch
Meli ya kivita ya UkrainePicha: picture-alliance/ITAR-TASS

Tangazo la kupeperushwa kwa bendera za katika vituo vya kijeshi katika mjini Crimea la afisa wa juu kabisa wa jeshi Jenerali Valery Gerasimov lilisema mpaka sasa wanadhibiti maeneo yote ya kijeshi katika eneo hilo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo bendera ya Urusi kwa hivi sasa inapepea katika katika vituo vyote 193 vya kijeshi mjini Crimea. Taarifa ya mkuu huyo iliongeza kusema bendera zilipandishwa katika hafla iliyoambatana na uimbaji wa wimbo wa taifa.

Shirika la habari la RIA novosti limemnukuu kamanda Gerasimov akiesema wale wanajeshi wa Ukraine wanaotaka kuondoka katika eneo hilo wako huru kufanya hivyo kwa kutumia usafiri wa reli na watajizaja nafasi hizo mara moja pale itakapobainika hawapo kazini. Ameongeza kusema kiasi ya wanajeshi 1,500 wa Ukraine ambao wamekuwa wakifanya kazi katika serikali ya Ukraine, katika kituo kilichopo mjini Simferopol kwa ajili ya kuandaa safari yao.

Maandalizi ya jeshi la Ukraine

Naye kaimu rais wa Ukraine, Oleksandr Turchynov ameliomba bunge la taifa lake kupitisha idadi fulani ya wanajeshi ambao watashirikia mazoezi ya pamoja na jeshi la Umoja wa kujihami wa NATO, kwa lengo la kuweka uwiano ulio sawa na jeshi la Urusi katika eneo la Crimea.

Ukraine Interim Präsident Alexander Turtschinow 23.02.2014 2013
Rais wa Mpito wa Ukraine Alexander TurtschinowPicha: picture-alliance/Itar-Tass/Maxim Nikitin

Ombi hilo la Turchynov linaelezwa kutokana na tangazo hilo la Urusi la kudhibiti vituo vyote vya kijeshi katika eneo la Crime. Kiongozi hiyo amesema Ukrine itafanya awamu mbili za mazoezi ya kijeshi na Marekani katika kipindi cha msimu wa kiangazi.

Serikali ya Marekani mwezi huu ilipendekeza kutumia asilimia 28 katika bajeti yake ya wizara ya ulinzi katika jitihada za kubadili mfumo wa kijeshi kuwa wa kisasa nchini Ukraine na katika mataifa mengine yalikuwa katika muungano wa kisovieti wa zamani.

Katika hatua nyingine, Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema maafisa wa uhamiaji nchini Ukraine wamewazuia wahudumu wa ndege ya abria ya Urusi kutoka katika ndege hiyo baada ya ndege hiyo kutua mjini Kiev. Taarifa hiyo imesema kitendo hicho ambacho hakukutolea taarifa za kina kina hatarisha usalama wa abiria. Kwa mujibu wa kanuni za usafiri marubani na wahudumu wa ndege za abiria wanapaswa kupumzika kabla ya kuanza safari nyingine.

Mapema wiki hii, wizara hiyo ilitoa taarifa iliyosema kwamba raia wa Urusi wamekuwa wakiwindwa nchini Ukraine na kuulalamikia utawala wa Ukrain kwa kutokuwa na uwezo au nia ya kutaka kuvizuia vitendo hivyo. Urusi imekuwa ikitumia ripoti inayosema watu wenye asili ya Kirusi nchini Ukraine wapo katika kitisho jambo ambalo limeonekana kama sababu ya kulitwaa eneo la Crimea.

Mwandishi: Sudi Mnette AFP/RTR
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman