Urusi yamuonya Pashinyan dhidi ya kuharibu mahusiano
25 Septemba 2023Urusi imeongeza kuwa waziri huyo mkuu wa Armenia ndiye wa kubebeshwa lawama kwa mgogoro wa Nagorno-Karabakh, kwa sababu alidanganywa na ahadi za mataifa ya Magharibi.
Hayo ni baada ya Pashinyan kuituhumu Urusi kuwa imechangia pakubwa katika kushindwa kwa wapiganaji wanaotaka kujitenga huko Nagorno-Karabakh. Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmity Peskov amesema:
"Mazungumzo yanaendelea katika ngazi mbalimbali. Pamoja na Armenia, haswa katika wakati huu mgumu. Hivi majuzi kulikuwa na mazungumzo ya simu kati ya Putin na Pashinyan. Tunaelewa hisia kubwa zilizopo wakati huu, lakini hatukubaliani kabisa na jaribio la kuitupia jukumu Urusi au vikosi vya walinda amani wa Urusi, ambao wanaonyesha ushujaa wa kweli katika kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa mamlaka waliyo nayo."
Hayo yakijiri, maelfu ya wakimbizi ambao idadi yao imepindukia 4,800 kutoka eneo hilo linalozozaniwa wameendelea kuwasili nchini Armenia.
Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev amefanya mazungumzo JUmatatu na mwenzake wa Uturuki Recepp Tayyip Erdogan, wakijaribu kuutafutia suluhu mzozo huo.
Aliyev ameahidi kulinda haki za jamii ya Waarmenia katika eneo la Nagorno-Karabakh.