Urusi yalaani Putin kufananishwa na Hamas
20 Oktoba 2023Biden alisema siku ya Alkhamis (Oktoba 19) Hamas na Putin wanalingana na wote wanalenga kuangamiza mataifa ya jirani zao wenye demokrasia.
Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov, alisema siku ya Ijumaa (Oktoba 20) kauli kama hizo hazifai hasa kwa wakuu wa nchi wanaowajibika.
Soma zaidi: Biden: Kufanikiwa kwa Ukraine na Israel katika vita vyao ni muhimu kwa usalama wa Marekani
Msemaji huyo alionya kwamba tishio kwa raia wa Urusi litaongezeka mara tu Israel itakapoanzisha operesheni yake ya ardhini kwa lengo la kulitokomeza kundi la Hamas linalotawala Ukanda wa Gaza.
Peskov hakubainisha ni nani atakayeiwakilisha Urusi katika mkutano wa kilele wa amani mjini Cairo utakaojaribu kuutafutia suluhu mzozo wa huko Gaza.
Soma zaidi: Biden aifananisha Hamas na Putin katika hotuba yake
Mkutano huo ulitarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi (Oktoba 21).
Israel imejibu vikali mashambulizi ya Hamas yaliyowauwa wa Israel 1,400 na hadi sasa mashambulizi hayo ya Isarel yameshauwa karibu 4,000 kwa upande wa Palestina.