1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

Urusi yakanusha njama ya kumuua mkuu wa Rheinmetall

12 Julai 2024

Msemaji wa ikulu ya Kremlin leo amekanusha kuhusika kwa Urusi katika njama ya kumuua mkuu wa kampuni ya utengezaji silaha ya Ujerumani Rheinmetall.

https://p.dw.com/p/4iEmm
Mkuu wa kampuni ya utengezaji silaha ya Ujerumani Rheinmetall Armin Papperger
Mkuu wa kampuni ya utengezaji silaha ya Ujerumani Rheinmetall Armin PappergerPicha: Thomas Trutschel/photothek.de/AA/picture alliance

Kampuni hiyo imetengeneza silaha muhimu ambazo Ujerumani inazipeleka Ukraine.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moscow, Dmitry Peskov amesema hawezi kutoa tamko kuhusiana na tuhuma hizo akidai kuwa ripoti iliyotolewa na shirika la habari la Marekani la CNN haiwezi kuchukuliwa kwa umuhimu kwa sababu vyanzo vyake havikuwekwa wazi.

Soma pia: Rais Putin akutana na Spika wa Bunge la Tanzania

Kulingana na ripoti hiyo ambayo kwa sasa imeandikwa pia katika gazeti la Ujerumani la Süddeutsche Zeitung, maafisa wa intelijenzia wa Marekani mapema mwaka huu walifichua mipango ya serikali ya Urusi ya kumuua afisa mkuu mtendaji wa Rheinmetall Armin Papperger.

Ripoti hiyo imezusha ghadhabu Ujerumani huku waziri wa usalama wa ndani Nancy Faeser akisema serikali inakichukulia kitisho cha Urusi kwa "umuhimu mkubwa."